GET /api/v0.1/hansard/entries/1193889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193889,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193889/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gataya",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13584,
"legal_name": "Mwenda Julius Gataya",
"slug": "mwenda-julius-gataya"
},
"content": "Bw. Spika, nimekagua orodha hii kwa makini. Majina ambayo yako hapa ni ya waheshimiwa kutoka Seneti na Bunge la Taifa ambao wanaheshimika sana. Sen. Mungatana, MGH, ni mchapakazi. Amekuwa katika Mbunge takribani miaka 15. Kwa hivyo, anayo tajiriba ya kutosha na tunatazamia kwamba uwakilishi wake utatufaa sisi kama Maseneta wa nchi ya Kenya. Sen. (Prof.) Kamar ambaye anasifika kote nchini. Pia kuna Mhe. Rahab Mukami, Mhe. Joseph Kalasinga Majimbo na Mhe. Esther Muthoni Passaris ambao wana uzoefu wa kutosha. Tunajua kwamba watatuletea sifa katika shughuli zao za kuwakilisha Seneti katika Bunge la Afrika. Bw. Spika, naunga mkono na tunawatakia mema katika safari yao ya kutuwakilisha katika Bunge la Afrika."
}