GET /api/v0.1/hansard/entries/1193915/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193915,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193915/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Thang’wa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda. Nilikuwa namtazama rafiki yangu Sen. Mungatana, MGH, wakati tulipokuwa tunapigania kuwa wenyekiti wa Kamati. Alikuwa ametulia vilivyo. Sikujua, alielewa alipokuwa anaelekea. Wahenga wa Kisasa watasema “ukiona vyakimya basi jua vyatarajia.” Nawapongeza walioteuliwa kuiwakilisha Kenya katika Bunge la Africa. Sen. (Prof.) Kamar, ametueleza kwamba kila nchi husika inateua wabunge watano kuwa wawakilishi katika Bunge la Afrika. Sheria la kuwateu wawakilishi wa Bunge la Afrika linasisitiza kuwa angalau mmoja wa wawakilishi hao lazima awe mwanamke. Kenya imeonelea ni vyema kutuma wanawake zaidi kuliko wamaume. Inanonyesha kuwa nchi hii ya Kenya inatilia maanani uongozi wa wanawake. Bunge la Afrika linaagiza lazima kuwe na mwakilishi mmoja wa kike lakini sisi tunawapeleka watatu. Nawasihi kwamba watakapokuwa katika Bunge la Afrika, wasimamie Kenya vilivyo ndio angalau ionekane kweli wanawake wakipata fursa wana uongozi wa hali ya juu. Walioteuliwa, Sen. Mungatana, MGH na Sen. (Prof.) Kamar wanauzoefu wa kazi hii kwa sababu wamekuwa wakihusika sio tu kwa kutunga sheria pia katika uongozi wa Serikalini katika upande wa utendaji kazi. Nina imani kuwa wawili hawa wana uwezo mkubwa wa kuwakilisha Kenya katika utenda kazi wao kulingana na tajiriba walionayo. Naunga mkono Hoja hii. Nina imani kuwa tutaipitisha."
}