GET /api/v0.1/hansard/entries/1193924/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193924,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193924/?format=api",
"text_counter": 271,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi leo nizungumze hapa kwa sababu ni muda mrefu sana tangu nizungumzie ndugu zangu ambao nimefanya kazi nao. Mhe. Sen. Mungatana, MGH, tulikuwa naye Serikalini mbeleni tukiwa wachanga sana. Ni kiongozi ambaye tunamheshimu sana. Wakati atakuwa katika Bunge la Afrika, kazi yake itakuwa nzuri sana. Atakuwa mwanachama wa timu ambayo inaenda pale kushughulikia masuala ya Bunge la Afrika kutoka nchi ya Kenya. Bw. Spika wa Muda, Sen. (Prof.) Kamar ni mama ambaye tunamheshimu. Mimi nina historia naye kwa sababa mimi nimekuwa hapa Bungeni kwa zaidi ya miaka 20. Kwa hivyo, nimeona vile alikuwa kwenye kiti cha usipika na kazi yake yenye heshima na vile tunavyomheshimu. Ndugu yangu wa tatu ni Mhe. Kalasinga. Mhe. Sen. (Dr.) Khalwale, unamjua. Miaka mitano iliyopita, mimi nilikuwa naibu wa kiongozi wa chama cha Ford Kenya. Ninakumbuka nikienda kule Bungoma kumfanyia kampeini Mhe. Kalasinga. Ni shukrani sana kuona kwamba amerudi Bungeni kwa sababu nilikuwa sijajua na tena amepewa nafasi hii kwa sababu yeye ni mchanga. Hajakaa Bungeni miaka mingi na ameanza kujizoesha. Kwa hivyo, ni elimu nzuri kwake kisiasa kwenda kule nje kutetea masuala ya Afrika. Wale wote ndugu zetu ambao wameenda kutuwakilisha ningependa wajue Afrika yetu iko na mambo mengi lakini ni bara lenye uwezo mkubwa. Waafrika ni watu ambao wanafanya kazi ngumu na kwa bidi sana. Barani Afrika tuna rasilimali ya kutosha. Ningependa Mhe. Sen. Mungatana, MGH, pamoja na Mhe. Sen. (Prof.) Kamar, mkiwa pale, mjaribu kuwauliza wenzetu wa Afrika ni vipi tunaweza kutumia rasilimali zetu ili tufaidike kama Bara la Afrika. Hata ukiona tuna rasilimali chungu nzima, kila wakati bara letu la Afrika linakubwa na changamoto nyingi. Tuko na mafuta, dhahabu, shaba na kila kitu lakini changamoto nyingi. Tunamwuuliza Mwenyezi Mungu awasindikize vizuri mwende pale mkafanye kazi nzuri. Mnajua bendera ya Kenya inapaa sana. Mhe. Sen. Mungaana, MGH, unajua wakati mmoja nilikuwa naibu wa Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni wa nchi ya Kenya. Tukiwa pale, Mkenya akizungumza unapata waafrika wengi wanasema haya mambo nyinyi mnayajua namna gani. Nilikuwa ninawaambia ni kwa sababu tumesoma vizuri na tuna mwelekeo fulani wa kisiasa na kiuchumi. Ningependa kuwasihi mjitahidi mhakikishe bendera yetu imeendelea kupepea vizuri na mtuletee matunda ambayo yataweza kuonyesha kuwa Kenya ni nchi ambayo inaendelea vizuri yenye amani na demokrasia halisi. Nyinyi mtaenda represent na kufanyia kazi Wakenya wote. Mkiwa pale, msije mkaanza tena kusema, “sasa huyu chama chake ni kipi.” Sasa nyinyi ni Wakenya na mwende na mfanye kazi nzuri."
}