GET /api/v0.1/hansard/entries/1193971/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1193971,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193971/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13592,
        "legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
        "slug": "onyonka-richard-momoima"
    },
    "content": "Inaonekana mtandao uko na shida hapa. Asante, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kumshukuru Sen. Kibwana kwa kuleta Hoja hii kwa Seneti. Ni jambo la heshima. Sisi kama viongozi, na hata kwa wale ambao ni madaktari kama Sen. (Dkt.) Khalwale, hatujayapa maswala ya afya ya kiakili umuhimu unaohitajika. Hatujachambua hili swala ili tuweze kujua kile kinachowaumiza kina mama wakishajifungua watoto. Ukiangalia runinga au magazeti, utaona visa vya kina mama ambao wanaua watoto wao. Jambo ambalo linasikitisha ni kwamba, utasikia Wakenya wakisema kuwa mama ambaye ameua mtoto wake alikuwa ni mwendawazimu. Watu wengine wanabaki wakishangaa kuwa yule mama alikuwa na shida gani. Shida ni kuwa hatujaona umuhimu wa kushughulikia afya ya kiakili. Ingekuwa vizuri kama vile huu Hoja unavyopendekeza, turudi mashinani na kujiuliza kile ambacho"
}