GET /api/v0.1/hansard/entries/1193973/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1193973,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1193973/?format=api",
"text_counter": 320,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13592,
"legal_name": "Onyonka Richard Momoima",
"slug": "onyonka-richard-momoima"
},
"content": "kinafanya Wakenya wengi kuwa na shida ya kiakili. Ningependa kumwuliza Sen. Kibwana kuongezea Hoja hii na kuhusisha maneno ya kielimu. Lazima tufahamishe wanafunzi katika shule zetu kuhusu afya ya kiakili. Shida ya afya ya kiakili imechangia wanafunzi wengine kuingia katika uraibu wa kunywa pombe, kutumia madawa ya kulevya na hata kujihusisha na vita vya kijinsia. Ingekuwa vizuri kama magavana na wawaakilishi wa bunge za kaunti wangeweza kuangalia Hoja kama hii kwa minajili ya kutafuta suluhu ya jambo hili la afya ya kiakili. Najua uoga ambao huletwa na Hoja kama hii. Utasikia watu wakisema ya kwamba hatuna wafanyikazi wa kutosha. Wengine nao watasema ya kwamba serikali za kaunti hazina pesa za kuwalipa wafanyikazi ambao watatibu wagonjwa wenye shida za kiakili. Sidhani shida yetu ni pesa. Shida yetu ni ugavi sawa, uwazi na uwajibikaji wa zile pesa kidogo ambazo tunazo. Tukiwajibika vilivyo, tutaweza kusuluhisha hili jambo. Hili ni swala nyeti na mimi naunga mkono. Wakati ambapo Hoja hii itakuwa Mswada na kuwasilishwa hapa, tutaongezea yale ambayo tuko nayo na pia tutamwuliza Sen. Kibwana mapendekezo yake ili tuboreshe Mswada huu zaidi. Natoa shukrani zangu kwake, Sen. Kibwana, kwa kufikiria hili jambo. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}