GET /api/v0.1/hansard/entries/1194263/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194263,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194263/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi nzuri ya kuchangia mjadala ulioko hapa wa kufanyia marekebisho Katiba ili hazina ya NG-CDF iweze kuingia katika Katiba na tuzuie wale wachache ambao wanataka kuvuruga hazina hii ambayo inafanya kazi nzuri nchini kote. Haitasahaulika kwamba tulipoanzisha ugatuzi nchini, mathumuni haswa ilikuwa ni kwamba ni vipi basi tutapeleka hela karibu sana na mwananchi wapate kujisimamia, kupata miradi na kufanya mambo ambayo yatabadilisha maisha yao. Ni kweli kuna mambo fulani ambayo yamegatuliwa na mengine yalibaki katika Serikali ya kitaifa. Sisi Wabunge tumebaki na majukumu makubwa ya kuangalia kwamba Serikali ya kitaifa inafanya kazi kufikia mwananchi aliye chini sana ama aliye mbali sana na Nairobi. Wenzangu wamesema kwa kirefu sana kwamba hazina ya NG-CDF inasaidia. Kwa kweli ukizunguka kona zote za nchi na maeneo Bunge yote, miradi utakayoona utafikiria kwamba pesa za NG-CDF ndio pesa za ugatuzi zinazofikishwa mashinani. Kuna hela nyingi sana lakini bado unakuta asimilia kubwa ya pesa ambayo inaenda kwa kaunti, inaenda kusimamia pesa za kulipa wafanyikazi, r ecurrent expenditure . Lakini hazina hii ya NG-CDF, miradi inaonekana kwa sababu asilimia tano pekee yake ndio inaotumika kulipa wafanyikazi, kumaanisha asimilia 95 inaenda kwa miradi kama vile kusaidia wanafunzi wetu. Kwa hivyo, asilimia 95 inaenda moja kwa moja kwa wananchi ili waweze kubadilisha hali yao ya kimaisha. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}