GET /api/v0.1/hansard/entries/1194264/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194264,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194264/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": "Kwangu kule Wundanyi tuko na changamoto tele. Lakini kwa sababu hali ilivyokuwa kabla ya ugatuzi, tulibaki nyuma muda mrefu. Ninakumbaka hazina ya Equalization Fund ilikuja kuleta usawa nchini, lakini tumeona kuwa ile hazina haijaweza kumea miguu. Imebaki tu kwenye daftari, iko kwa vitabu, iko kwenye Katiba, lakini haijafikia maeneo ambayo yana changamoto nyingi maeneo yaliobaki nyuma. Lakini hazina ya NG-CDF kuna shule kadhaa pale kwangu ambazo hazikuwai ona shilingi hata moja ya pesa za kitaifa kabla ya ugatuzi au NG-CDF kuja. Leo hii tumeboresha shule zetu, tumejenga shule mpya, tumeweka miundo misingi kwa shule nzuri kupitia hii hazina. Tukisikia kwamba kuna mahakama inapinga ama inasema kwamba NG-CDF sio muhimu na ikiwezekana itolewe na ikiwezekana ipelekewe magavana. Kile kinachoibuka kisheria maswala tunayo simamia ya NG-CDF hayajagatuliwa. Wakati mahakama inasema kwamba kazi hiyo inaweza kufanywa na kaunti tunashindwa kuelewa ni vipi basi kazi ambayo haijagatuliwa, itafanywa na magavana na wale Members of CountyAssemblies (MCAs). Nikija katika suala la wanafunzi ambao hufadhiliwa na hazina hii, kule kwangu nina shule moja inaitwa Mbela High School. Iko maeneo kame ya Kishushe. Katika shule ile, asimilia 60 ya wanafunzi waliopo pale wako na ufadhili wa mia kwa mia kutoka kwa hazina ya NG-CDF. Asilimia 60 wanategemea NG-CDF pekee yake. Tunawalipia karo yote maanake ni sehemu ambayo imekauka sana, ina shida na changamoto nyingi. Leo hii shule iko karibu kufungwa, maanake kama asilimia 60 ya mapato ya shule kupitia karo, inatoka kwa hazina ya NG-CDF. Wakati haiko wale wanafunzi wako nyumbani. Shule haijielewi itafunga ama itafanya namna gani. Kwa hivyo, lazima tuliangazie suala hili sana. Sasa hii tuko na janga la ukame na njaa, lakini swala ambalo ni la kitaifa na ambalo linaingiza Wakenya uoga ni hili swala la kusemekana kwamba hazina ya NG-CDF haitakuwa. Kule kwangu watu wengi ni wakristo na kila asubuhi ninapata simu za wachungaji na wakristo, pamoja na waislamu walioko pale Wundanyi wakisema wanalivalia njuga suala hili kwa maombi. Wanaona kama NG-CDF haitakuwa, basi maisha yao yamekorogeka. Sasa kila asubuhi ninapata simu ya wachungaji wakiniambia kwamba wanafunga na kuomba, na Bunge la Kitaifa liweze kusimama kidete ili Mungu aliye juu awezeshe Kenya hii ijue kwamba NG- CDF ni muhimu, ijue kwamba wananchi wanaumia, ijue kwamba wanafunzi hata wale wanaoanza kuenda vyuo vikuu wanaumia pia. Mwaka huu watoto wa vyuo vikuu wengi wameenda shule. Lakini karibu 50 imebidi wahairishe kuingia university kwa sababu walikuwa wanategemea NG-CDF. Lakini kwa sababu NG-CDF imecheleweshwa na kukorogwa, imebidi wengine tumewashika mkono kwa kutumia marafiki na sisi wenyewe kibinafsi, lakini wengi wameshindwa kuingia university, kwa sababu ya hazina hii. Kwa hivyo, kama kuna jambo moja ambalo sisi Wabunge tunastahili kushikana kwa umoja ili wakati sheria hii inapokuja kupigiwa kura hapa Bungeni, sisi wote 349 tuwe ndani ya Bunge, tupitishe jambo hili. Lile linalonitia moyo kabisa ni kwamba pesa hizi zimekuwa ni kidogo mno. Sasa yatakikana tuiweke iwe asilimia 5 na tuambie wananchi ya kwamba tuko tayari kama Wajumbe wao kutetea mambo ambayo wanayabeba moyoni. Na ninawahakikishia wale ambao wanasema kwamba NG-CDF ni pesa ambayo inawafaidi Wabunge hawajasoma sheria, hawajui regulations za kusimamia hazina hii. Hakuna shilingi ya NG-CDF ambayo inaenda kufaidi Mbunge yeyote aliye kwenye Bunge la Kitaifa. Mara nyingine ninasikia hata wenzetu Waseneta wanasema mambo ambayo hawana uhakika nao. Wanasema kwamba tuwape hazina yao kufanya oversight kwa sababu Wabunge wako na NG-CDF. Wanakosa kujua NG-CDF sio ya Mbunge, bali ni ya wananchi. NG- CDF mia kwa mia haimufaidi Mbunge. Tunashukuru mungu Bunge hili linatuangalia vizuri. Tuko na mileage, tuko na mshahara kwa hivyo hatuhitaji kuchungulia hazina ya NG-CDF kufaidi familia na mifuko yetu. Wenzetu wa Seneti wanatakikana wafahamu kwamba tunapowatetea The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}