GET /api/v0.1/hansard/entries/1194269/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194269,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194269/?format=api",
    "text_counter": 241,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Wundanyi, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Danson Mwashako",
    "speaker": null,
    "content": ". Wanatakikana waelewe na wasome sheria ya NG-CDF kuwa hizi pesa sio zetu ni za wananchi. Lakini mkisema kwamba wanataka kuangalia pesa zinatumika vipi nchini, basi hata wanapopata oversight funds hata Mbunge was eneo Bunge, Mbunge wa akina mama wanatakikana pia wawezeshwe ili tuweze kufanya oversight yetu sawasawa. Ninamalizia, Mhe. Spika wa Muda, kwa kuunga mkono Hoja hii. Hata zile pesa za hazina ya akina mama, ile tunaita National Affirmative Action Fund (NG-AAF), pia kwa kweli wanafanya kazi kubwa. Pale kwangu, Mheshimiwa wangu, Mhe. Haika Mizighi, amesimama kidete na makundi yaliosahaulika akina mama na vijana. Ninaomba kwamba wakati tunapitisha hazina ya NG-CDF kufika asilimia tano tuongeze na ya akina mama ili Mbunge wa eneo Bunge anapofanya kazi na yule anayesimamia maswala ya akina mama naye afanye kazi ya kueleweka ili nchi yetu yote isonge mbele na tufaidike kama nchi nzima. Mhe. Spika wa Muda, ninasema asante. Ninaunga mkono mabadiliko haya ya Katiba. Asante."
}