GET /api/v0.1/hansard/entries/1194324/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194324,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194324/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Leo najitoa kimasomaso kuunga mkono mjadala huu wa kurejesha mgao wa NGAAF na ule wa NG-CDF. Mpaka sasa hivi tunavyojadili swala hili hapa Bungeni, tuna watoto ambao hawajaenda shule na wazazi wao wanaishi katika hali duni za umasikini. Ningependa kumweleza jaji ambaye aliondoa mgao huo kwamba ikawa alipata maisha mazuri na kuweza kusomeshwa na kupata cha mchana hadi cha jioni lakini, kunao watu katika Taifa hili wanao matatizo mengi sana. Tumeona Wabunge ambao wamepata mgao huu wa NG-CDF wakijenga shule. Pia wamekuwa wakitoa bursary kila mwaka. Tumeona wengi wamefanya maendeleo makubwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}