GET /api/v0.1/hansard/entries/1194325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194325,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194325/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "sana huko mashinani. Na inafahamika kwamba pesa hizi si za Wabunge bali ni za wananchi walala hoi. Ndio maana mimi kama Mama Zamzam nasema kuwa itakuwa muhimu sana ikiwa sisi Wabunge tutalijadili swala hili hapa kwa kina na kwa utulivu na kulishughulikia mara moja ili ikifika mwisho wa mwezi huu, watoto wetu na wazazi wao wawe na furaha kurudi shuleni. Wazazi wafurahie kupata wanafunzi wamekaa katika madarasa mazuri. Wengi wetu sisi tulizaliwa katika familia maskini. Nakumbuka tulikuwa twabeba samadi na maji kutoka nyumbani kwenda kutengeneza madarasa shuleni. Tulishukuru sana mgao huu ulipo anza kwa sababu mambo yalikuwa shwari sana. Madarasa yamekuwa yakijengwa kwa kasi sana. Kunazo sehemu zilizoko mashinani zaidi ambazo mgao huu haujawafikia, ingekuwa ni vyema sana zikifikiwa ili tuone watoto wa Turkana, Pokot, Miroroni na Mwakirunge wakikaa maisha mazuri na wakipata elimu ya kutosha. Kunao watoto ambao wamehitimu shule za msingi na wanataka kujiunga na shule za sekondari lakini mpaka sasa, hawajafanya hivyo kwa sababu ya hali duni ya maisha ya wazazi wao. Hivi ambavyo mgao huu umesitishwa, watoto hawa bado wanasubiri. Ningependa kuiuliza Serikali, watasubirisha watoto hawa mpaka lini? Tutawanyima haki zao kama wananchi wa Kenya mpaka lini? Ni dhahiri kwamba hali inazidi kuwa ngumu Kenya kwa sababu sisi pia tunawafanya wananchi kuishi maisha magumu. Kwa mfano, nikirejeleea pesa za Wabunge wanaowakilisha akina mama za NGAAF, pesa hizi zimesaidia wanawake wengi sana kuinua biashara zao, kujikimu kimaisha na wengi hata kupata pesa za kulisha familia zao, kusomesha watoto na pia kulipa ushuru nchini. Leo hii tunapowanyima mgao huu wa NGAAF, nina imani kuwa wengi wamekaa manyumbani. Hata hapa nilipo, wengi wanapiga simu na kuniambia: ‘Mama Zamzam, tulikupigia kura tukiwa na matarajio makubwa sana kwako. Ulituahidi vitu vingi sana kama vile maendeleo na biashara lakini mpaka sasa ni kimya tu.” Hili ni jambo la kusikititsha sana maana akina mama wamekuwa wakipanga foleni kutupigia kura na kuchagua viongozi bora watakaoleta maendeleo mashinani. Lakini, mpaka sasa, mfuko ambao ulikuwa unawasaidia na kuhakikisha kuwa ule msichana wa Pwani aliyeachwa katika mila na tamaduni ambazo zilimfanya asipate elimu, alikuwa amepata mwanya mzuri wa kusoma. Leo hii amerudi nyumbani na pengine, anatafutiwa mume aolewe kwa sababu hana pesa za kumwendeleza kimasomo. Ikiwa tutataka wanawake tufikie thuluthi tatu katika Bunge hili, ni dhahiri shairi kuwa pesa hizi ni muhimu sana zirudi kwenye mifuko ya Wabunge ili tufikie malengo ya kupata viongozi, madaktari na waalimu watakao saidia kujenga taifa hili. Si wote wanaotoka katika familia za kitajiri ndio wanaweza kuwa madaktari na marais tu. Mtoto wa maskini pia akiwezeshwa anaweza fikia ndoto hizo. Kwa mfano, mimi mama Zamzam nimelelewa maisha ya shida sana. Ilikuwa ni mtihani hata kupata sare na viatu vya kwenda skuli. Wakati huo, hapakuwa na mtu wa kutusaidia. Mara nyingine, mama alikuwa ananipa simsim na sambusa nikauze kwa wenzangu na kwa majirani ndio nipate karo na pesa za kununua vitabu na mahitaji mengine. Lakini sasa, tulikuwa tumerahisisha mambo katika familia duni kupitia migao hii ya NGAAF na NG-CDF. Ushauri wangu ni tuweze kurejesha pesa hizi ili wananchi waweze kupata manufaa."
}