GET /api/v0.1/hansard/entries/1194326/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194326,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194326/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Kwa upande mwingine, tumekuwa tukishuhudia ukatili wa kijinsia. Wanawake wamehangaishwa sana na wengi wameuliwa katika mikono ya waume zao. Kama kina mama, tulikuwa tumezindua mfumo mzuri wa kujenga centres za gender-based violence . Vituo ambavyo vinawapa akina mama wakati wa kuweza kujifikiria na kutoa maamuzi tofauti maishani. Lakini sasa hivi, kwa mfano, kituo cha Mwakirunge Kaunti ya Mombasa kimesimamishwa kwa sababu hatuna mgao wakukiendeleza. Hata jana na juzi kwenye Kaunti ya Mombasa, kuna mwanamke amepigwa na kudungwa kisu na mumewe mpaka akafa. Kuna wanawake wanaouliwa kinyama na mimi kama mama Zamzam siwezi kuwachukua wanawake hawa wote na kuishi nao katika nyumba yangu. Ilikuwa ni dhahiri kuwa pesa hizi zingejenga vituo ambavyo akina mama wangewekwa kwa muda mfupi, kuwezeshwa kufanya biashara na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}