GET /api/v0.1/hansard/entries/1194617/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194617,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194617/?format=api",
"text_counter": 171,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Harisson Kombe",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, isingekuwa hazina hii, sijui Magarini ingekuwa wapi. Nilipochukua hatamu ya uongozi wa eneo Bunge la Magarini mwaka wa 2003, tulikuwa na shule mbili za upili peke yake. Niliweza kutumia hazina ya maendeleo katika Maeneo Bunge na nikaziinua kutoka shule mbili hadi shule 27. Kufikia sasa, tumejenga shule 25 mpya za sekondari. Tulikuwa na waliohitimu na shahada za ualimu wakiwa ni watu watatu peke yake ndani ya eneo Bunge la Magarini lakini kufikia mwaka wa 2007, idadi hiyo ilikuwa imeongezeka hadi watu 400."
}