GET /api/v0.1/hansard/entries/1194618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194618/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Harisson Kombe",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, tukiangazia maeneo bunge mengine wakati huo ilikuwa wazi na hakukuwa na vizuizi vingine. Tuliweza kujenga zahanati za kutosha katika kila kata. Vilevile, tuliwapeleka wanafunzi kusomea udaktari. Hivi tunavyozungumza, lengo na shabaha ni kuweza kuwa na chuo cha ukulima ndani ya Magarini, ambacho kinajengwa na hazina ya maendeleo katika Maeneo Bunge. Tukiangazia elimu ya wasichana wetu, tumenuia kujenga shule mpya ya wasichana kule Marafa, ambayo itakuwa ni shule ya kisasa na siku za usoni itakuwa shule ya kitaifa. Kwa pande zote na kwa hali yote, hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ni hazina ambayo haistahili kuchezewa hata kidogo. Mtu yeyote anayepinga hazina hii, kwa lugha fupi, huyo ni mchawi wa maendeleo na anastahili kunyongwa. Ashindwe shetani!"
}