GET /api/v0.1/hansard/entries/1194619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194619/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Magarini, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Harisson Kombe",
"speaker": null,
"content": "Mhe. Spika wa Muda, hiyo asilimia tano iliyopendekezwa na ndugu hawa ninaweza kusema haitoshi kwa sababu kuna mambo ya dharura ambayo huzuka, haswa baa la njaa; na kama hatungekuwa na hazina, ingebidi tutegemee Serikali kuu. Moja kwa moja, ingekuwa ni kuingia katika mfuko wa hazina ya maendeleo ya Maeneo Bunge na tuweze kuwanunulia chakula watu wetu. Hivyo basi, ukifika wakati wa kurekebisha, nitapendekeza kuwa asilimia 7.5 itengewe hazina ya maendeleo ya Maeneo Bunge ndiyo tuweze kupata angalau shilingi milioni tano za kusimamia majanga maana siku hizi mambo mengi huzuka na kutatiza wananchi wetu. Mhe. Spika wa Muda, ningependa kukomea hapo nikisema asante tena kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Hoja hii."
}