GET /api/v0.1/hansard/entries/1194646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194646,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194646/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Likoni, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda. Kongole kwa kupata fursa ya kutuongoza katika Bunge hili la 13. Kwanza, nawapongeza Wabunge wenzetu wawili kwa kuileta Hoja hii ya marekebisho ya Katiba ili tuweke sheria ya NG-CDF, NGAAF na hata fedha za Seneti kwenye Katiba. Ni muhimu sana kuweka hazina hizi katika Katiba. Hii ni kwa sababu Katiba ndio sheria kubwa kushinda sheria zingine zote katika taifa letu la Kenya. Kumekuwa na kesi nyingi sana ambazo kila wakati zinapinga kuweko kwa hazina hizi. Kwangu mimi ndizo zimezingatia ugatuzi ambao umefika mpaka kule mashinani hadi kiwango cha wadi na hata vijijini. Ukiangalia miradi inayotekelezwa kupitia hazina inamilikiwa na wakaazi wa maeneo bunge yale ama kaunti zetu 47 utaona kwamba kabla ya miradi kubuniwa ama kutekelezwa, Wakenya hupewa nafasi ya kutoa mapendekezo ya miradi wanayoihitaji. Ukiwauliza Wakenya kuhusu faida za ugatuzi ambazo zinawafikia kupitia serikali za kaunti na hazina za NG-CDF na NGAAF, watakuambia kwmba faida asilimia mia kwa mia zinatokana na hizi fedha. Kwa wanafunzi wengi ambao walitaka kuendelea na masomo katika shule za upili, ukosefu wa karo ulikuwa kikwazo na changamoto kubwa kwao kabla ya kubuniwa kwa hazina hizi. Takriban zaidi ya miaka 20 iliyopita, wakati ambapo hatukuwa na hazina hizi, Wakenya katika sehemu nyingi humu nchini hawakuweza kuona barabara za lami katika maeneo walikokuwa wakiishi; hakukuwa na madarasa ya kisasa, na hakukuwa na ufadhili wa karo ya shule. Sasa jiulize, je, fedha hizi zilikuwa zinaenda wapi ama kutumika vipi? Hizi ni fedha ambazo mwananchi wa chini amemiliki, kwa hisani ya hazina hizi, na anatoa mapendekezo yeye mwenyewe kuhusu miradi ambayo angependa itekelezwe kwa manufaa yake. Pesa za NGAAF zinaangalia makundi ya Wakenya waliotengwa kama vile The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}