GET /api/v0.1/hansard/entries/1194647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194647,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194647/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Likoni, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Mishi Mboko",
"speaker": null,
"content": "walemavu, akina mama na vijana ambao wametengwa sana kutoka nyanja za kiuchumi katika taifa letu. Pia, walemavu na akina mama wameweza kuboresha hali zao za kiuchumi kupitia njia tofauti za kibiashara, upande wa sanaa na kukuza vipaji vyao. Kwa hivyo, hazina hizi ni lazima ziwekwe kwenya Katiba ndio tusihangaishwe kila saa na kesi zisizo na maana na kupoteza muda wa kuwahudumia Wakenya. Hivi sasa, watoto wetu wanahitaji karo za shule. Wengi wao wako nyumbani. Sisi kama Wabunge tumekuwa na kazi kubwa sana. Imekuwa kizungumkuti. Kila wakati tunaambiwa kuwa tutapata fedha hizi, mara tunaambiwa si haki kulingana na sheria. Haziko katika sheria. Kwa hivyo, tunataka kufanya marekebisho na kuweka sheria hii katika Katiba. Katiba ni sheria mama na hatutakuwa tena na kizungumkuti ama sintofahamu kuhusiana na fedha hizi. Hata kule kwangu Likoni nimejenga shule ya upili ya waschana mahali ambapo hapukuwa na shule ya upili, haswa ya bweni. Watoto wa kike, ambao kwa muda mrefu wametengwa katika mambo ya kielimu ama kimasomo, wameweza kufika shuleni. Tumeweza kuboresha mambo ya usalama na mambo ya mazingira. Tumeweza kuboresha pia mambo ya sanaa na ya michezo. Hata majanga yanapokuja, pesa za NGAAF na NG-CDF zimesimamia na kuhakikisha Wakenya wametolewa katika changamoto kama hizo. Kwa hivyo, yeyote anayepinga fedha hizo ni adui mkubwa wa maendeleo katika taifa letu la Kenya. Tutasimama kidete tuhakikishe kuwa Wakenya wameendelea kufaidika na fedha hizi. Pesa zao zitumike kwa miradi yao ili waweze kujiita Wakenya na wajivunie kuwa Wakenya. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}