GET /api/v0.1/hansard/entries/1194725/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194725,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194725/?format=api",
    "text_counter": 40,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kamukunji, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Yusuf Hassan",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": " Ningependa kuelezea umuhimu wa lugha hii. Lugha ya Kiswahili ni muhimu nchini, katika Afrika Mashariki, Afrika na Ulimwengu wote. Ni lugha yetu ya mama na ya kiasili tunayojivunia; sio lugha ya kigeni, ya mkoloni au ya mbeberu, bali ni lugha yetu ya kitaifa, ya kitamaduni ya Kenya na Mwafrika. Lugha hii inazungumzwa na Wakenya wengi zaidi kuliko lugha yoyote ile. Asilimia themanini na tano ya Wakenya, ambao ni watu karibu milioni arubaini na mbili, wanazungumza lugha hii. Mbunge anapokuwa katika pilka pilka za uchaguzi, na hata alipokuwa akitafuta kura kwa wananchi, hakuwa anazungumza lugha anayoitumia hapa Ukumbini ya kibeberu na ya kikoloni. Alikuwa anatumia lugha ambayo mama mboga na watu wa kawaida wanazungumza – lugha tunayo jivunia na ambayo ina umuhimu duniani – Kiswahili. Kiswahili kinatambuliwa na kuzungumuzwa katika Afrika Mashariki katika nchi kama vile Tanzania, Uganda, Msumbiji, Somalia, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia, visiwa vya Komoros na Ushelisheli. Unapotembea katika nchi hizi, hautahitaji kutafuta mkalimani. Duniani na pia Marekani, zaidi ya watu laki moja wanazungumza lugha ya Kiswahili. Hivi majuzi, tulienda Uchina kwa matembezi kama wabunge, na tulishangazwa sana na Wachina wenye vyeo vikubwa katika Serikali vile walivyozungumza Kiswahili. Mabalozi wengi wanaotumwa katika nchi yetu… Sasa hivi ukizungumza na Balozi wa Japani, Uingereza na Ujerumani, utakuta kwamba ni wazungumzaji wa Kiswahili. Kwa hivyo, hii ni lugha ya kidiplomasia, utamaduni, sayansi; na ni lugha inatumika katika sehemu mbalimbali duniani. Hii ni lugha ambayo tunahitaji kuikuza na kuiendeleza. Ni lugha ya kipekee ya Kiafrika ambayo inazungumzwa kwa wingi zaidi duniani. Kuna watu 200,000,000 ambao wanaizungumza, na inatambuliwa kama lugha rasmi ya Umoja wa Mataifa, nchi za Afrika Mashariki na Afrika Kusini. Sasa hivi, Kiswahili kimeanza kufundishwa katika zaidi ya vyuo elfu mbili mbalimbali duniani, kwa mfano Havard na Oxford, ambapo watu wanafundishwa Kiswahili kama lugha muhimu duniani. Kiswahili kinatangazwa katika redio na televisheni mbalimbali duniani kama British Broadcasting Corporation (BBC), Voice of America (VOA), vituo vya redio vya Urusi, Uchina na India."
}