GET /api/v0.1/hansard/entries/1194728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194728,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194728/?format=api",
"text_counter": 43,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Japan. Hakuna nchi iliyojiendeleza kwa kutumia lugha ya kibeberu. Kwa hivyo, Kiswahili ni lugha ya ukombozi, haswa ukombozi wa kifikira, na kitatupeleka mbele. Pia, Kiswahili kimetumika katika mapambano ya kuondoa ubeberu na ukoloni mamboleo katika maisha na hali ya kila siku ya Mkenya na Mwafrika. Hili lilifanyika ili tuweze kupata uhuru kamili wa kifikira na kuzatiti mila, utamaduni na fikira zetu za kiasili za Kiafrika. Tunahitaji kukuza Kiswahili kama msingi wa maendeleo yetu ya kibinadamu. Tukifanya hivyo, tutatambuliwa, tutaheshimiwa, kutukuzwa na kuwa na utu kamili katika dunia hii, ikiwa tutakuwa na fahari ya kuendeleza na kutumia lugha yetu. Mwisho, Kiswahili kinatumika kuleta umoja, ushirikiano, mashikamano na undugu katika Nchi ya Kenya. Sisi ni watu wa makabila mbalimbali hapa Kenya, lakini jambo moja ni kwamba ukienda Turkana, Kwale, Moyale ama Marsabit na kwote ulipo, Kiswahili kinatuunganisha, na ni lugha ya umoja na maendeleo. Badala ya kusambaratika kupitia tofauti za kikabila, Kiswahili ni daraja inayo tuunganisha na tunasafiri pamoja kama Wakenya. Kenya itakuwa na nguvu zaidi ikiwa tutazatiti na kulinda lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha yetu ya kiasili. Ningependa kuwaomba Wabunge wenzangu kuwa tubuni Baraza la Kiswahili ambalo litazindua sheria, mipango na utaratibu wa kuendeleza Kiswahili. Baraza hili litakuza, litaimarisha na kujenga lugha yetu muhimu ya Kiswahili. Tuwe na fahari, uwezo na tujikomboe kiakili na kifikira; na pia tuzatiti lugha hii katika sheria, maendeleo na maisha ya Wakenya. Baraza la Kiswahili litachangia na kusaidia katika kukuza Kiswahili na Afrika. Itaimarisha umoja wa Afrika Mashariki na Afrika kuu katika mapambano ya lugha na maendeleo duniani. Kwa hivyo, nawashukuru na ningependa tuunge mkono kwa kubuniwa Baraza ka Kiswahili la kitaifa. Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa fursa hii."
}