GET /api/v0.1/hansard/entries/1194734/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194734,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194734/?format=api",
"text_counter": 49,
"type": "speech",
"speaker_name": "Laikipia Kaskazini, JP",
"speaker_title": "Mhe. Sarah Korere",
"speaker": null,
"content": " Shukrani, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuafiki Hoja hii na kumpongeza Mhe. Kaka Yusuf kwa kuwakilisha Bungeni Hoja ya kutaka Bunge hili kupendekeza kuundwa kwa Baraza la Kiswahili katika nchi yetu tukufu ya Kenya. Ukitazama Sura ya pili, kifungu cha saba moja katika Katiba ya nchi yetu, kinasema kwamba lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kitaifa. Pili, Katiba inaendelea kusema kwamba Kiswahili na Kingereza ni lugha rasmi. Kwa hivyo, kwanza ni jambo la busara kutilia maanani lugha yetu ya kitaifa ambayo ni Kiswahili; kisha lugha rasmi ambayo ni Kiswahili na Kingereza. Nilitazama wakati Wabunge wa Kaunti wakiapishwa, na nikaona dada mmoja ambaye katika mitandao ya kijamii, aliweza kukejeliwa na kudhihakiwa sana kwa sababu ya kushindwa kuchukua kiapo kwa lugha ya Kimombo. Inatakiwa ifahamike kwamba huwezi pima akili, busara na hekima ya mtu kupitia lugha ya Kimombo. Nilipokuwa natazama kanda ile, nilijiuliza swali. Iwapo Mfalme William angeapishwa kwa lugha ya Kiswahili, je dhihaka na kejeli zingekuwa kama zile tulizoshuhudia yule mwanadada akidhihakiwa? Ningeomba Wabunge wenzangu na taifa letu la Kenya kwamba lazima tukikuze Kiswahili, na tuwe na fahari yetu, ambayo ni Kiswahili."
}