GET /api/v0.1/hansard/entries/1194736/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194736,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194736/?format=api",
    "text_counter": 51,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Leo ukienda Uingereza, Waingereza wanazaa kwao Uingereza wanakuza na kuwafunza watoto wao Kiingereza, na sisi twataka kupima hekima zetu kulingana na lugha ambayo si yetu. Ukienda Ufaransa, ni vile vile. Wanafunzi wetu wanapoenda kusoma Ujerumani, sharti kwanza wasome lugha ya Kijerumani ili waweze kufunzwa kwa Kijerumani. Kwa hivyo, litakuwa jambo la busara sana kama sisi Wakenya na wanajumuia wa Afrika Mashariki kuweza kujivunia na kukikuza Kiswahili kama fahari yetu. Hii ni muhimu ili wengine wanapokuja kusoma katika Bara la Afrika na haswa katika Kanda ya Afrika Mashariki, sharti waweze kujifunza lugha yetu ya Kiswahili. Wakenya wengi, haswa wale ambao labda hawajasoma vile, ama hawana mazoea ya lugha hii ya Kimombo, wameweza kutapeliwa katika biashara ya mashamba kwa sababu ya kutia sahihi katika mambo ambayo hawaelewi. Iwapo mawakili wetu watakuwa na mazoea ya kuandika hata mikataba katika lugha ya Kiswahili, watu wataweza kuelewa vilivyo ni nini wanatia sahihi."
}