GET /api/v0.1/hansard/entries/1194737/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194737,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194737/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Tukizungumzia mambo ya ukoloni, twajivunia kwamba tumepata uhuru. Lakini, bado kuna ukoloni mamboleo. Akili zetu bado hazijakombolewa. Tunaamini sana mambo ya nje kuliko yale ambayo tuko nayo hapa ndani. Ninatoka Laikipia. Katika miaka hio ya ukoloni, mkoloni aliita mzee mmoja Maasai, akatia sahihi kitu ambacho kiliandikwa kwa lugha ya Kimombo, na ardhi yetu yote ikachukuliwa. Kama huo mkataba ungeandikwa kwa lugha ya Wamaasai, labda huyo mzee hangelipeana ardhi yetu bure. Naomba Wabunge wenzangu, Wakenya wazalendo na wanakanda wa Afrika Mashariki, iwapo tutaimarisha mahusiano yetu, lazima tuwe na lugha ambayo inatushikanisha. Lazima tujikomboe na zile fikira za kikoloni za kufikiria kwamba kuzungumza Kiingereza kingi ndivyo kujua. Hata wale ambao wanazungumza lugha za kiasili, wao bado wanajua. Wabunge wenzangu ambao wameketi hapa watakubaliana nami kwamba ni nadra sana watoto wetu kuzungumza kwa Kiswahili. Mtoto akifika miaka miwili, ameanza kuzungumza kwa Kiingereza. Kiswahili ni nadra; lugha ya mama hamna tena. Kwa hivyo, hii ni Hoja muhimu sana. Naomba Wabunge waiunge mkono ili tuweze kubuni baraza la Kiswahili, tukuze nchi yetu, mahusiano na uhusiano wetu wa Kanda ya Afrika Mashariki."
}