GET /api/v0.1/hansard/entries/1194742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194742,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194742/?format=api",
    "text_counter": 57,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi Kaskazini, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Nafurahia sana leo kwamba katika Bunge hili mwanzo, tumeanza vizuri na lugha yetu ya Kiswahili. Hoja ambayo tunaizungumzia leo ni kuhusu hii lugha yenyewe. Kwa muda mrefu, taifa la Kenya limeachwa nyuma na mataifa ya Afrika Mashariki katika maneno ya lugha ya Kiswahili. Tanzania imekuwa mstari wa mbele. Pia, Zanzibar imekuwa msitari wa mbele. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, akija hapa Kenya, anaongea lugha safi ya Kiswahili ilhali sisi wenyewe bado tunaongea Kiingereza katika mikutano mikubwa kama yeye yuko. Rais Paul Kagame wa Rwanda huongea kwa Kiswahili akija hapa Kenya. Lakini sisi wenyewe katika ile mikutano yuko, tunaongea Kiingereza. Ni muhimu tujue kwamba lugha ya Kiswahili ni unganishi katika Afrika Mashariki. Vile Baraza la Afrika Mashariki linazidi kuongezeka—sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeingia na mataifa mengine yanaingia—ni vizuri tuwe na lugha ambayo inaweza kuunganisha Afrika Mashariki, na lugha hiyo ni Kiswahili. Ni vizuri taifa hili la Kenya libuni Baraza la Kiswahili ili hiki Kiswahili tunachoongea kiwe ambacho kinaeleweka. Hatuna baraza la lugha ya Kiswahili hapa Kenya. Kila wakati Kiswahili kinadhihakiwa. Unasikia mara watu wametoa maneno mapya, mara kinakuwa"
}