GET /api/v0.1/hansard/entries/1194744/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194744,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194744/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kombokombo. Hakikuwi katika ile itikadi ya Kiswahili yenyewe. Unasikia kila mtu anaongezea maneno yake, kwa sababu hakuna baraza. Katiba ya Kenya inatambua kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa, lakini ukienda kwa ofisi ya Waziri ama uende kwenye idara zetu za kitaifa, utapata kwamba yule anayeongea Kiswahili hatasikizwa. Yule atakayeongea Kiingereza ndiye atasikizwa, ilhali hawa wote ni Wakenya na lugha ya Kiswahili inatambuliwa katika Katiba. Tukiwa na baraza kuu la Kiswahili hapa Kenya, hii lugha ya Kiswahili itatambulika katika maofisi. Leo hii, Mkenya akienda kwenye ofisi ama mahakamani, anaandikiwa stakabadhi zake zote kwa Kiingereza, ilhali yeye haelewi hiyo lugha. Akiingia ndani ya korti, yule hakimu naye anaongea kwa Kiingereza. Hivyo basi, Mkenya ambaye yuko katika taifa lake ambalo lina lugha asilia ya Kiswahili anashindwa kuendeleza kesi yake kwa lugha anayoitambua, ilhali hii lugha inatambuliwa kwenye Katiba. Hili baraza litahakikisha kuna mahakama ambazo ukitaka kuendeleza kesi yako kwa Kiswahili, unaenda huko an ukitaka kesi yako iendelezwe kwa Kiingereza, unaenda mahakama ya Kiingereza. Mahakimu na mawakili watashurutishwa na hili baraza kwamba lazima wawe wanajua Kiswahili sanifu. Leo hii ukienda katika hii shule ambayo inafundisha mawakili hapa Kenya, utaona wale mawakili wengi wanaanguka mitihani kwa sababu ya lugha ya Kiingereza, ilhali wako na lugha yao ambayo wanaweza kutumia kuendesha taratibu za korti. Jambo lingine muhimu ni kwamba Kiswahili ama lugha yoyote huwa ni ya kuendesha biashara. Afrika Mashariki ikiwa na lugha moja, biashara hapa kwetu itanoga, na kila mtu atakuwa na nafasi ya kufanya biashara bila kuwa na pingamizi. Kila mtu atakuwa na nafasi ya kufanya biashara bila kikwazo cha lugha. Leo hii, ukitaka kwenda kufanya biashara Sudan Kusini, utapata shida sana kwa sababu hamutaelewana kilugha. Lakini iwapo Afrika Mashariki yote itatumia lugha moja ya Kiswahili katika mawawsiliano, biashara katika nchi hizi itazidi kudumishwa, na watu watapata manufaa."
}