GET /api/v0.1/hansard/entries/1194746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194746,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194746/?format=api",
"text_counter": 61,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Siku hizi, utapata kuwa wazazi wanafahamu Kiswahili na pia lugha za mama, lakini watoto hawajui lugha hizi, na wanazungumza Kiingereza peke yake. Kina nyanya wanapowatembelea, wanatatizika kuwasiliana na wajukuu kwa sabau wajukuu wanazungumza Kiingereza ambacho mara nyingi kina nyanya hawakifahamu. Mara nyingine, mama ni Mkikuyu na baba ni Mjaluo, lakini badala wafunze watoto Kiswahili, wanawafunza Kiingereza. Basi mababu wanapowatemebelea, wanashindwa kuzungumza na wajukuu. Utapata watoto wanakosa itikadi na nidhamu kwa kuwa hamna lugha ambayo wanaweza kutumia katika mafunzo na mababu wao."
}