GET /api/v0.1/hansard/entries/1194754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194754/?format=api",
"text_counter": 69,
"type": "speech",
"speaker_name": "Seme, ODM",
"speaker_title": "Mhe. (Dkt.) James Nyikal",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii. Ninaunga mkono Hoja hii ya kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya kwa sababu ya shida moja kubwa kuliko shida yoyote nyingine tuliyonayo hapa Kenya. Shida hii ni kutoongea lugha moja. Pengine ni ukabila umetuzuia kuendeleza nchi hii yetu ya Kenya. Tukiweza kumaliza shida hizi, Kenya itaendelea. Tunahitaji chombo ambacho kitaunganisha Kenya iwe kitu kimoja. Tukiwa na lugha moja ambayo sisi sote tunazungumza itatusaidia. Ukiangalia vyama vyetu vya siasa, vyote ni vya ukabila. Watu wakiajiriwa kazini, wao huajiriwa kwa misingi ya kikabila. Katika ofisi za serikali, pia watu wameajiriwa kwa misingi ya kikabila. Kwa sababu hii, tunarudi nyuma. Kwa hivyo, chombo ambacho kitatuleta pamoja, kitasaidia sana. Kama chombo hicho kitakuwa ni kubuni baraza la Kiswahili hapa Kenya, basi nami ‘nafunga’ mkono Hoja hii. Mimi ‘nafunga’ mkono."
}