GET /api/v0.1/hansard/entries/1194766/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194766,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194766/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dagoretti Kusini, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. John Kiarie",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, ningependa nifahamishwe na nijue kama Mjumbe wa Seme yuko hakika kwenye Kanuni zetu za kudumu anapokejeli taaluma kama uigizaji. Hilo ni kwa sababu anaposema kwa njia ya kudhalilisha kwamba leo hatuko hapa kuleta drama . Drama ninavyoifahamu ni kuigiza. Na hakika uigizaji ni taaluma ambayo inaheshimika nchini. Wengine wetu tumekuzwa na taaluma hii ya uigizaji. Kwa hivyo, singependa taaluma hii ya uigizaji idhalilishwe na Mjumbe huyu wa Seme anaposema kwa kejeli kwamba leo hatuko hapa kufanya drama . Drama kwa Kiswahili ni uigizaji ama sanaa ya uigizaji. Mheshimiwa Spika, ningependa nijulishwe kama huyu Mjumbe yuko mbali na Kanuni zetu za kudumu anapodhalilisha taaluma ya maana kama hii ya uigizaji. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}