GET /api/v0.1/hansard/entries/1194771/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194771,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194771/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kweli itaendeleza Kenya hii? Haiwezekani. Kwa sababu hiyo, ni muhimu sana tutafute njia ya kuunganisha Wakenya wote ili wawe kitu kimoja. Na kama ni lugha ya Kiswahili itakayofanya hivyo, basi tuendelee njia hiyo. Mimi sikatai; tumeendelea kukuza Kiswahili iwe lugha muhimu. Kiswahili kiko katika Katiba yetu. Sivyo? Tena, hata shuleni watoto sasa wanafundishwa Kiswahili vizuri kushinda wakati sisi tulikuwa shuleni. Sasa ukienda Nyanza, usifikiri utapata watoto wanazungumza Kiswahili vile mimi ninazungumza hapa. Watashinda hata wale watoto wanaotoka Pwani. Na juzi tu, mtoto ambaye aliongoza kwa Kiswahili nchini si alitoka Maranda? Hiyo ni sawa na hakuna neno."
}