GET /api/v0.1/hansard/entries/1194772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194772,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194772/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Siku hizi tumetambua kuwa Kiswahili ni miongoni mwa mahitaji ya masomo unapoingia kazini, na hata katika vyuo vikuu. Zamani tulikuwa tunahitaji Kiingereza na Hesabu peke yake, lakini sasa tunahitaji Kiingereza au Kiswahili na Hesabu. Si tumeendelea? Si lazima tuendelee kufanya hivyo ili Kiswahili kiwe na umuhimu ambao unatakikana na utaonyesha ni lugha yetu. Wengine husema ni lugha ya mama, lakini si ya akina mama wote. Akina mama wengine hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Hata Afrika au dunia nzima, watu wengi wanazungumza Kiswahili. Kwa hivyo, hata tukitaka kuunganisha Afrika nzima, ile lugha ambayo itatusaidia ni Kiswahili. Ukienda East na Central Africa, karibu nchi zote zinazungumza Kiswahili. Tunajua Tanzania inaongoza. Ukienda DRC, Rwanda, Burundi na Central African Republic, sote zinaongea Kiswahili. Kwa hivyo, tukitafuta ile lugha ambayo itaunganisha Afrika nzima, itakuwa ni Kiswahili. Unajua udhaifu mkubwa sana wa Afrika nzima ni kutokuwa pamoja. Tujenge lugha, pia tujenge barabara na uchumi ili watu watembee Afrika yote. Ukitembea nchi yoyote, kile kitu unahitaji sana ni lugha. Kwa hivyo itakuwa rahisi ikiwa watu wote Afrika watazungumza lugha ya Kiswahili. Watu watatembea, watafanya biashara na Afrika itakuwa kitu kimoja. Nguvu ya nchi ni watu kuwa wengi. Kama Afrika ingekuwa pamoja na sisi sote kuwa kitu kimoja, tungeendelea. Ukienda nchi kama India, imeendelea kwa sababu ina watu wengi. China ina watu wengi; Russia ina watu wengi. Kwa hivyo, tunahitaji Afrika iwe na umoja na watu wake wazungumze lugha moja. Napendekeza hiyo lugha iwe Kiswahili. Hata hapa, tuko na Kiswahili katika kitabu chetu cha Kanuni za Kudumu za nidhamu. Na hili lilikuja mwaka jana tu. Tunaendelea vizuri. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, naunga Hoja hii mkono kwamba tubuni baraza la Kiswahili la taifa la Kenya. Asante sana."
}