GET /api/v0.1/hansard/entries/1194779/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194779,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194779/?format=api",
    "text_counter": 94,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Imenti Kaskazini, Huru",
    "speaker_title": "Mhe. Rahim Dawood",
    "speaker": null,
    "content": " Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuzungumza. Baadhi ya Waheshimiwa wengine wanafikiri kuwa siwezi kuzungumza Kiswahili. Ningependa kumpongeza Mhe. Daktari Nyikal vile ameweza... Tukiwa kwenye mkutano na ndugu yangu, TJ Kajwang’, alisema kuwa wao hawajui hii lugha, na wanakumbana na changamoto nyingi sana. Nakubaliana na Mhe. Yusuf kuhusu kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Kwa kweli, wakati huu tusipoboresha Kiswahili, sijui ni lipi tutakuwa tukifanya. Watu wengi katika maofisi ya kiserikali hawajui kuzungumza Kiswahili. Wafanyikazi hawa hushindwa kuwasaidia wale ambao hawajui Kizungu. Labda kule Nyanza ndiko wanazungumza Kizungu kuliko Kiswahili. Kenya nzima tunafaa kujivunia lugha ya Kiswahili, kwa sababu tunaweza kuiongea mahali popote. Mhe. Nyikal amesema mambo ya Uhindi, lakini hajafahamu kwamba kule wanazungumza lugha zaidi ya elfu moja. Hata Uchina labda kuna lugha aina tofauti. Lakini ni muhimu lugha yetu ya Kiswahili itumiwe katika nyanja zote, haswa katika ofisi za Serikali. Ukienda town, watu huzungumza Kiswahili tofauti kulingana na mahali wametoka. Ukienda kwa duka la Mhindi, atakuongelesha Kiswahili ambacho hautaelewa. Ukienda Eastleigh, Kiswahili cha Msomali ni tofauti. Naomba tuweze kubuni baraza hili ili watu wote wafunzwe Kiswahili sanifu, na tuweze kuboresha mawasiliano."
}