GET /api/v0.1/hansard/entries/1194780/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194780,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194780/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Imenti Kaskazini, Huru",
"speaker_title": "Mhe. Rahim Dawood",
"speaker": null,
"content": "Kama vile, Mhe. KJ ametuelezea mambo ya drama, ni muhimu baraza hili libuniwe ndio kila mtu aweze kufunzwa Kiswahili shuleni. Siku hizi ukienda shuleni, utapata ubaoni wameandika kwa Kizungu peke yake. Tunafaa kuwaweka watoto wetu maanani, na kitu cha kwanza ni lazima wafunzwe Kiswahili kisha waendelee na Kizungu huko mbele. Wizara ya Elimu na Kamati ya Elimu hapa Bungeni zinafaa kuangalia kwamba watoto wakiwa wachanga kabla wafike gredi ya nne, wasifunzwe Kizungu peke yake. Inafaa wafunzwe Kiswahili pia, ndio kila mtu hapa nchini aelewe Kiswahili. Namshukuru Clerk wetu, bwana Kirui, kwa sababu tukiwa naye katika Kamati ya kutengeneza Kanuni za Kudumu, yaani"
}