GET /api/v0.1/hansard/entries/1194784/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194784,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194784/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Moiben, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Phylis Bartoo",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii. Ningependa kumpatia kongole Mhe. Hassan kwa kuleta Hoja hii ya Kiswahili hapa Bungeni. Katika vifungu vya 7 (1) na (2) vya Katiba ya Kenya, lugha ya Kiswahili imepewa kipao mbele katika taifa la Kenya, haswa matumizi yake. Kwa mfano, Kiswahili kimetambuliwa kama lugha ya taifa la Kenya. Katika vyuo vikuu vya kitaifa na shule za sekondari, Kiswahili pia kimepewa kipao mbele. Ndipo sasa tunahitaji baraza la Kiswahili, ili liweze kushughulikia lugha ya Kiswahili ipasavyo. Tukitengeneza baraza la Kiswahili hapa Kenya, litaweza kushughulikia mambo mengine ambayo hayajatambuliwa. Nimesikiza kwa makini vile Mhe. Hassan amepiga debe, na vile Wabunge wenzangu wamechangia. Hii inamaanisha kwamba sasa ni wakati mwafaka wa kupeleka Kiswahili kiwango kingine. Sitaki kusema mengi, ila kumpatia Hassan kongole, na kuwasihi Wabunge wenzangu kuunga mkono Hoja hii ndio Kiswahili kiendelee mbele. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}