GET /api/v0.1/hansard/entries/1194788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194788,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194788/?format=api",
    "text_counter": 103,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sigor, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Peter Lochakapong",
    "speaker": null,
    "content": "Najua kwamba wengi wetu katika Bunge hili hutumia lugha ya Kiswahili tunapoomba kura na tunapokutana na watu wetu kule vijijini. Sisi hutumia Kiswahili tunapowasiliana na wakazi katika maeneobunge na kuwasilisha hoja zetu. Lugha ya Kiswahili ni muhimu kwa sababu inawawezesha watu kuelewa ni nini hasa tunachowaambia. Ndio maana namshukuru Mheshimiwa Yusuf Hassan kwa kuileta Hoja hii na ndiposa naiunga mkono. Jambo lingine muhimu ni kwamba lugha ya Kiswahili inaunganisha watu wa Afrika Mashariki. Watu wa Afrika Mashariki watakapoungana, itakuwa rahisi kufanya biashara na majirani wetu. Mhe. Spika wa Muda, umesikia kuwa watu wengi, hata humu Bungeni, wanasema kwamba lugha ya Kiswahili ni ngumu kwa sababu Kiswahili ambacho tumezoea kuzungumza ni kile ambacho tunatumia tunapoomba kura kule nyanjani. Lugha ambayo watu wanaamini sana si Kiswahili sanifu. Kwa hivyo, tunapokuja hapa na kusema kwamba ni wakati wa kila mtu kuzungumza Kiswahili sanifu, hali hiyo huleta utata kidogo na wengi wetu tunasema kwamba lugha hiyo ni ngumu. Hiyo ndio sababu kuu zaidi ya kubuni Baraza hili la Kitaifa kupitia Hoja hii – ili wale watakaopewa nafasi ya kuendeleza lugha hii waweze kutoa mwongozo ambao utatusaidia sisi sote kujifunza Kiswahili vizuri ili tuweze kuwasiliana na watu wetu kwa njia bora zaidi. Tunapowasiliana na Wakenya ambao tunawakilisha hapa Bungeni huwa tunatumia lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, tukiendeleza lugha ya Kiswahili katika taifa hili, tutawaleta Wakenya wote pamoja tunapowasiliana nao kwa lugha ambayo wanaelewa. Ikiwa Wakenya wataelimishwa kuhusu sera za Serikali kwa lugha ambayo wanaielewa, itakuwa rahisi sana kwao kuiunga mkono Serikali. Wenzetu katika mataifa jirani tayari wamebuni mabaraza ya Kiswahili. Inaonekana sisi tumechelewa kidogo. Sisi, viongozi tulioko hapa, tukiipa lugha ya Kiswahili kipaumbele, viongozi wengine Serikalini watatuiga na kuendeleza Kiswahili kwa njia moja ama nyingine. Jambo hili litachangia kuwepo kwa uzalendo katika taifa letu kwa sababu sisi sote, kama"
}