GET /api/v0.1/hansard/entries/1194790/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194790,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194790/?format=api",
"text_counter": 105,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "viongozi, pamoja na wale tunaowaongoza, tutakuwa tunaongea kwa lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, naomba sisi sote tujitahidi kuzungumza kwa Kiswahili. Tukipata nafasi yoyote ya kuhutubia wananchi, tufanye hivyo tukitumia lugha ya Kiswahili, ikiwezekana, ili watu wetu pia waige mfano huo. Sote tunapoongea kwa Kiswahili, tutaweza kuiendeleza lugha hii. Tarehe saba, mwezi wa saba ni siku ya Kiswahili duniani. Hiyo ni siku ambayo imetengwa kwa ajili ya lugha yetu ya kitaifa ili dunia nzima iweze kuitambua. Kiswahili kitawaunganisha wakazi wa Afrika Mashariki na bara zima la Africa. Kama viongozi, tunapaswa kuendeleza na kukikuza Kiswahili ili tusonge mbele. Nawahimiza viongozi wote katika Serikali wawaelimishe Wakenya kuhusu sera za umma wakitumia lugha ya Kiswahili. Wakenya wanaielewa lugha hiyo. Nashukuru sana kwa sababu Bunge letu limeweza kuchapisha Kanuni za Bunge – The"
}