GET /api/v0.1/hansard/entries/1194796/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194796,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194796/?format=api",
"text_counter": 111,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Katika kuendeleza elimu, Kiswahili ni lugha ambayo tungeweza kusaidia haswa wanafunzi ambao wamekuwa wazito katika kujua lugha ya Kiingereza ama wamekuwa na sintofahamu kuelewa mufti lugha ya Kiingereza. Iwapo pia tutaweza kuwafasiria kwa lugha ya Kiswahili, huenda wakaelewa zaidi na kubobea katika masomo yao. Nchi jirani za Rwanda, Uganda na Burundi haziko karibu sana na Tanzania lakini wameweza kukuza Kiswahili katika kiwango cha juu. Leo sisi Kenya na Tanzania ni kama mtoto wa mjomba na shangazi ama kama pua na ndevu maanake tuko hapo kwa hapo, sako kwa bako. Kwa hivyo, ni lazima tukuze lugha hii ili iweze kupata wasifa kama lugha zingine. Leo ukienda Ujerumani utapata wanaongea kijerumani na wana elimu na wanatukuza lugha yao. Ukienda Ufaransa, utapata wanaongea Kifaransa na wana elimu na wanatukuza lugha yao. Kwa hivyo, sisi pia ni lazima tutukuze lugha yetu. Tunapotukuza Kiswahili na kukiboresha, tutaweza kuboresha tamaduni zetu pia. Kiswahili kimechukua pia lugha za Kibantu na hapa tena katika taifa letu la Kenya tumeona lugha nyingi ni za Kibantu. Maneno fulani ya Kibantu yemechukuliwa na kuwekwa kwenye Kiswahili. Maneno ya Kiarabu pia yamechukuliwa na yameunganishwa pale ndiposa tumeweza kupata hii lugha ya Kiswahili."
}