GET /api/v0.1/hansard/entries/1194797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194797/?format=api",
    "text_counter": 112,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, tukiweza kuitukuza na kuipa kipaumbele, tutaweza kuwa na mabadiliko mengi sana. Zaidi ya watu milioni 200 ulimwenguni wanaongea lugha ya Kiswahili, na lugha ya Kiswahili ni lugha tamu! Unajua, kuzungumza Kiswahili pia si kuzungumza tu, ni lazima utoe ile lafudhi na ile sauti, kwa Kiingereza tunayosema ni the tone, lakini kwa Kiswahili ni lafudhi; na sauti ni lazima iwe inaambatana na lugha hii, basi unapoizungumzia utasikia ni lugha tamu sana. Hata ukizungumza kwa ile lafudhi ya sawa katika mambo yetu ya kinyumbani, mambo ya kimapenzi, unaona ni lugha ambayo inatoa ushawishi na inatoa furaha na bashasha kuliko lugha nyingine. Naona Mhe. Didmus anacheka lakini kwa upande huo pengine ukinifuata ninaweza kukuelimisha zaidi ndiyo unielewe kinaga ubaga ninamaanisha nini. Kwa hakika sisi tunahitajika tuingie katika historia. Kama wenzetu wa Tanzania na Zanzibar wameweza kutengeneza baraza hili la Kiswahili na sisi ni wale wanaita kwa Kiiingereza the big brother ama wale makaka wakubwa katika jumuiya yetu ya Afrika Mashariki, tunatakikana kuwa sisi ndio tunaongoza katika mipango kama hii ili tuweze kuboresha muungano wetu na kuweza hata kuboresha mambo yale ya kisiasa ambayo yanahitaji kujumuishwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa wale ambao hawajaelewa, kwa Kiingereza ni Political Federation . Tukitaka kuiweka iwe sawia na sisi, ni lazima lugha ya Kiswahili iwe sawia. Kwa sababu hata tunapoomba kura, hapo ambapo tunatoa hotuba zetu za kisiasa tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Tunapokwenda kwa vyombo vya habari kuzungumzia sera, shabaha na malengo yetu, tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili. Na iwapo mambo mengi katika shughuli zetu za kijamii tunazungumza kwa lugha ya Kiswahili, kwa nini lugha hii tusiipatie kipaumbele? Kwa nini lugha hii tusiitukuze? Kwa nini lugha hii isiwe na baraza lake? Baraza hili pia litaweza kukuza ajira. Leo tuna Wakenya wengi ambao wamebobea, ni mahiri katika lugha ya Kiswahili lakini wamekosa ajira kwa sababu pengine nafasi za kuweza kuonyesha umahiri wao ama ugwiji wa lugha hii ya Kiswahili hakuna. Kwa hivyo, tukiwa na baraza kama hili linaweza pia kutengeneza ajira aina tofauti katika taifa letu. Tukiwa sasa tuko kwa ugatuzi tunajua kwamba itaenda mpaka kule mashinani ili watu wajue kwamba lugha hii sasa ni lugha ambayo unaweza kuizungumzia katika mahakama, utaweza kuizungumza katika zahanati kupata afya, utaweza kuizungumza katika taasisi yoyote ya umma ili uwe na wepesi na upatiwe nafasi, na umekuwa huru kuzungumza lugha hii. Kwa hivyo, mimi nataka nimwambie Mhe Yusuf kuwa kuleta Hoja hii kwa hakika ametufurahisha sote kama taifa la Kenya, na kwa hakika umetufunza lugha ambayo itaweza kufanya tamaduni zetu ziweze kuheshimika, si katika Taifa la Kenya pekee lakini katika bara"
}