GET /api/v0.1/hansard/entries/1194801/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194801,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194801/?format=api",
"text_counter": 116,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kimilili, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Didmus Barasa",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi kuchangia Hoja hii muhimu ya kuirai Serikali ibuni Baraza la Kiswahili la taifa. Ninakubaliana na Hoja hii na ninaiunga mkono kwa sababu Wakenya wengi hawajui lugha ya Kiingereza lakini kila Mkenya, mpaka hata marafiki wetu, kama vile Mheshimiwa T.J. Kajwang’, siku hizi wanazungumza Kiswahili sanifu. Kama alivyosema Mhe. Mboko, ni lazima Kiswahili kiwepo ama kitambuliwe na mashirika tofauti ya Serikali. Ninakubaliana na hilo. Ili tukikuze Kiswahili, naweza pia kumwomba Mhe. Mishi Mboko kwamba kuanzia leo, akiniandikia jumbe fupi katika WhatsApp asitumie Kiingereza kama kawaida yake, bali atumie Kiswahili. Vilevile, nimefurahi siku ya leo kwa sababu miongoni mwa wanafunzi walioko hapa ni binti wangu wa kwanza anayeitwa Chelsea Didmus, kutoka Shule ya Serare. Yuko pale ananiona. Wiki iliyopita alishinda akinifunza Kiswahili na nafikiri hilo ni jambo zuri sana. Ninampongeza Mheshimiwa kwa kuleta Hoja hii kwa sababu wapo wagonjwa wengi ambao wakienda kutafuta huduma za matibabu, pengine wanapata daktari ambaye hajui ama haelewi Kiswahili na mara nyingi wakienda kutibiwa wanazungushwa. Mara nyingi ukienda kutibiwa huwa unamueleza daktari sehemu za mwili ambazo zina maumivu. Kwa hivyo, inakuwa vigumu kwa daktari yule na mgonjwa kuwawasiliana vizuri. Kuwepo kwa Baraza la Kiswahili katika nchi ya Kenya itawalazimisha hata wale wanaotoka nchi za ughaibuni na kufanya kazi katika nchi yetu ya Kenya, kuenda skuli wakajifunze jinsi ya kuzungumza na kuelewa lugha ya Kiswahili, kama ilivyo desturi ya Wakenya wengi wanaofanya kazi katika nchi ambako Kiingereza hakizungumzwi. Wakenya wanapowasili katika nchi hizo, inawabidi wajifunze lugha zinazozungumzwa huko, kama vile Kifaransa, Uturuki au Kiarabu. Kwa hivyo, itakuwa ni vizuri nchi ya Kenya iwe na baraza kuu la lugha ya Kiswahili. Vile vile, tunaomba kuwa kandarasi nyingi za zabuni zitayarishwe kwa lugha ya Kiswahili. Kuna bidhaa ambazo mwananchi wa kawaida huenda kununua ilhali hazifahamu kwa lugha ya Kiswahili. Nilijua hivi majuzi tu kwamba spare parts ni vipuri kwa lugha ya Kiswahili. Nilikumbushwa na Mhe. Mishi Mboko. Kuna siku gari langu liliharibika nikiwa Mombasa. Nilipoenda kutafuta gear box na plugs ikawa ni matatizo matupu kwenye mawasiliano. Baada ya siku mbili, rafiki yangu mswahili alimueleza mwenye duka kwa lugha aliyoielewa kwamba nilitaka vipuri vya gear box ndio gari langu likatengenezwa. Nina hakika kwamba kama kungekuwepo na baraza la Kiswahili katika nchi ya Kenya, singesumbuka. Ningeenda tu kwa duka niseme ninataka kifaa fulani na mambo yangekuwa mazuri. Jambo la mwisho, na ambalo ni muhimu sana, ni kuziomba taasisi za Serikali zitilie maanani Hoja ambazo hujadiliwa na kupitishwa na Bunge la Taifa. Tukizungumzia Hoja tofauti tofauti, wakuu serikalini, wakiwemo mawaziri wanaohusika, wanastahili kuhakikisha kwamba masuala yanayojadiliwa na kupitishwa hapa Bungeni yanafuatiliwa na kutekelezwa. Ninashukuru kwa sababu tunaye Bwana Spika ambaye lugha yake ya Kiswahili imeanza kuwa sanifu sana. Atakuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kwamba Serikali ya Kenya inahakikisha kwamba Hoja tunayoizungumzia hivi sasa imeweza kutimizwa ili kila Mkenya popote alipo aweze kuzungumza Kiswahili. Vile vile, Kiswahili ni lugha ya taifa, na inazungumzwa katika nchi nyingi ulimwenguni. Nilishangaa hivi majuzi nilipokuwa katika taifa la Afrika Kusini, nilipokuwana na wananchi wa taifa hilo waliokuwa wakizungumza Kiswahili. Pia, nilikuwa katika nchi ya Congo, ambako nilikutana na Wakongo waliokuwa"
}