GET /api/v0.1/hansard/entries/1194803/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194803,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194803/?format=api",
    "text_counter": 118,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wakizungumza Kiswahili. Nimekuwa katika nchi ya Uganda, na Waganda pia wanazungumza Kiswahili. Kwa hivyo, ni lazima sisi pia, tukiwa nchi-mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, tukikuze Kiswahili kikiwa mojawapo ya lugha za kuimarisha umoja wa Afrika Mashariki. Mhe. Spika wa Muda, kuweko kwa Baraza la Kiswahili humu nchini kutatoa nafasi kwa wageni kutoka mataifa tofauti kama vile Ufaransa na Nchi za Umiliki wa Kiarabu ili waweze kujifunza, kuzungumza na kukikuza Kiswahili. Ningependa pia Serikali yetu ifuatilie utekelezaji wa pendekezo hili. Kwa mfano, kukiwa na kongamano za kimataifa, ni muhimu kuwe na wakalimani watakaokuwa wakitafsiri lugha ya Kiswahili kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa ili washikadau kutoka nchi hizo waweze kuelewa yanayojiri kwenye kongamano, na pia waweze kushiriki kwenye mahojiano yoyote yale kupitia usaidizi wa wakalimani hao. Tukihudhuria kongamano katika nchi ambako Kifaransa ndiyo lugha rasmi, kama vile nchi za Africa Magharibi, mazungumzo yote hufanywa kwa lugha ya Kifaransa na wakalimani hutafsiri kutoka lugha ya Kiingereza hadi kwa Kifaransa ama kutoka lugha ya Kifaransa hadi lugha ya Kiingereza ili wanaohudhuria kongamano hilo waweze kufahamu yanayojiri. Ningependa kuchukua nafasi hii kumpongeza, tena kwa dhati, Mhe. Yusuf kwa kuileta Hoja hii muhimu sana Bungeni. Kwa mara ya kwanza, nimemuona rafiki yangu, Mbunge wa Embakasi Kaskazini, Mhe. Babu Owino, akiwa amebeba Kamusi ya Kiswahili. Mhe. Mishi Mboko alipokuwa akizungumza, Mhe. Babu Owino alikuwa akipekua kamusi hiyo. Mhe. Babu Owino amekuwa akiwafunza wanafunzi wa Kidato cha Nne kupitia akaunti yake ya Facebook . Ninamuomba kuanzia kesho aanze kuwafunza kwa lugha ya Kiswahili. Kuna wanafunzi wengi humu nchini ambao hawaelewi kile kizungu chake kikubwa. Mhe. Mishi Mboko, ninakupongeza. Nakuomba umuorodheshe Mhe. Babu Owino kama mwanafunzi wako wa Kiswahili kwa kuwa Kiswahili chake ni kibovu sana na hakieleweki. Kwa haya yote, naiunga mkono Hoja hii."
}