GET /api/v0.1/hansard/entries/1194807/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194807,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194807/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, UDA",
"speaker_title": "Mhe. Dr. Robert Pukose",
"speaker": null,
"content": " Nashukuru, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niweze kuchangia Hoja ambayo imeletwa na Mhe. Yusuf Hassan, Mbunge wa Kamkunji. Lengo lake ni kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Lugha yetu ya Kiswahili ni safi. Itakuwa vyema lugha za Kiswahili na Kiingereza zikienda sambamba. Mambo mengi tunayoyafanya tunahitaji lugha itakayotuwezesha kufanya shughuli kadhaa wa kadha; haswa za kimasomo, kibiashara na kimatibabu. Mimi, kama daktari, mara nyingi napenda mgonjwa anieleze kuhusu ugonjwa alionao kwa lugha ambayo anaifahamu vizuri. Kuna watu ambao wanapoongea wanatumia lugha isiyoeleweka. Kizazi cha sasa kinatumia lugha ya mtaa ambayo inaitwa Sheng . Rafiki yangu, Mhe. Babu Owino na jirani yangu Mhe. Caleb Amisi, wanaongea lugha ya Sheng . Hawa vijana lugha yao ni sheng . Hivyo ndivyo tunapoteza lugha yetu ya Kiswahili. Lugha ya Sheng haieleweki miongo mwa Wakenya wengi na watu kutoka mataifa jirani. Inasemekana Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar…"
}