GET /api/v0.1/hansard/entries/1194823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194823,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194823/?format=api",
"text_counter": 138,
"type": "speech",
"speaker_name": "Endebess, UDA",
"speaker_title": "Mhe. (Daktari) Robert Pukose",
"speaker": null,
"content": " Ahsante, Mhe. Spika wa Muda. Lahaja ambayo Mhe. Babu anaongea ni Kiswahili ambacho hakijakuzwa kwa njia safi. Wanasema Kiswahili kilizaliwa kule Zanzibar na Tanzania. Kililelewa hapa Kenya, kikakufa kule Uganda na kikazikwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mimi ni jirani wa nchi ya Uganda. Kwa sasa, wameanzisha Kiswahili katika shule za msingi na sekondari. Kwa hivyo, Kiswahili kinaendelea kuamka sasa. Mhe. Hassan ameleta Hoja hii wakati unaofaa. Tukiwa na Baraza la Kiswahili la Kenya litashughulikia suala la kukizuza Kiswahili, na sio kulazimisha Kiswahili kitumike mahali ambapo hakifai. Baraza hilo litahakikisha kwamba Kiswahili kinachotumika ni nadhiri ama kinakubalika na kila mtu."
}