GET /api/v0.1/hansard/entries/1194826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194826,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194826/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. (Daktari) Robert Pukose",
    "speaker": null,
    "content": "Sisi, majirani wa Mhe. Kalasinga, tunaelewa akisema “ninakujako bwana”. Tunafahamu anakuja na anasema kwa njia nzuri. Lakini, mtu kutoka sehemu nyingine hataelewa. Tulipohudhuria michezo kule Tanzania, Wakenya tunapenda kusema ‘nipe’ kitu fulani, lakini Watanzania kwa lugha yao wanasema “tafadhali naomba”. Wakenya hatutaki kusema hivyo. Sisi tunasema “lete hii” na tunaona sio madharau. Lakini ukiambia Mtanzania “leta hii” hata kama ni kwa duka, anaona kama unmadharau. Kwa hivyo, ni lazima tujaribu kutumia Kiswahili sanifu, na kwa njia ambayo ni ya heshima, ili kila mtu aridhike katika nchi yetu."
}