GET /api/v0.1/hansard/entries/1194831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194831/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mandera Kusini, UDM",
    "speaker_title": "Mhe. Abdul Haro",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia fursa adimu niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa bungeni na Mhe. Yusuf Hassan, ambaye namshukuru sana. Hoja hii inaihimiza Serikali, kupitia vyombo vya dola husika, kuanzisha Baraza la Kiswahili. Hoja hii ni muhimu sana kwa sababu ya mambo kadhaa ambayo baadhi ya Wabunge wenzangu wamegusia. Mbali na kuwa lugha pekee ya Kitaifa, lugha ya Kiswahili pia huwa inatumiwa kama nembo ya umoja wa taifa, ama symbol of national unity kwa Kimombo. Pia lugha hii inazungumzwa na Wakenya wengi, hasa wale ambao wanaishi kule mashinani. Umuhimu wa Baraza la Kiswahili ambalo tunahimiza kubuniwa kupitia Hoja hii ya Mhe. Yusuf Hassan sio tuu litasaidia kukuza uenezaji wa uzungumzaji wa Kiswahiki katika Taifa hili, bali pia litasaidia katika kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili sanifu katika shule zetu."
}