GET /api/v0.1/hansard/entries/1194832/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194832,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194832/?format=api",
    "text_counter": 147,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mandera Kusini, UDM",
    "speaker_title": "Mhe. Abdul Haro",
    "speaker": null,
    "content": "Tusisahau kwamba somo la Kiswahili linahitajika, hasa wakati wanafunzi wanapotaka kuendelea na masomo katika taaluma zingine za juu. Kwa mfano, wanafunzi ambao wanataka kujifunza taaluma ya Kiswahili, somo la Kiswahili ni muhimu. Ni lazima uwe umefanya vizuri katika Kidato cha Nne ili uweze kuingia katika taasisi za kufunza taaluma ya ualimu. Hata wale ambao ni mawakili, tunafahamu kwamba lugha ya Kiswahili inahitajika katika taaluma hiyo."
}