GET /api/v0.1/hansard/entries/1194833/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194833,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194833/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mandera Kusini, UDM",
    "speaker_title": "Mhe. Abdul Haro",
    "speaker": null,
    "content": "Namshukuru Mhe. Yusuf Hassan kwa kuleta Hoja hii ya kusaidia kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili. Litakapobuniwa, Baraza hilo litachangia ukuzaji wa Kiswahili katika kuzungumza na pia itahimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli za kila siku serikalini. Kwa mfano, Bunge ama wizara za Serikali muhimu, zitatumia lugha ya Kiswahili kwa sababu hii ndiyo lugha ambayo inatumiwa na Wakenya wengi katika mawasiliano yao ya kila siku. Baraza la Kiswahili litasaidia kuhimiza matumizi ya Kiswahili sanifu katika taasisi zetu zote za elimu na ofisi zetu kama vile Bungeni na kwenye idara zinginezo. Baraza la Kiswahili pia litasaidia katika kutafsiri. Kwa mfano, litatafsiri ripoti ambazo zinatoka katika taasisi fulani, vitabu na pia sera za Serikali ambazo zinaweza kutumika mashinani na kueleweka vizuri na wananchi wetu wengi ambao wanategemea kuzungumza lugha ya Kiswahili."
}