GET /api/v0.1/hansard/entries/1194843/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194843,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194843/?format=api",
    "text_counter": 158,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hawajaenda shule na hawafahamu Kiingereza. Lugha mbadala ya kuweza kupata usaidizi katika ofisi ya Serikali ni lugha ya Kiswahili. Wananchi wanakuwa na changamoto kubwa, hasa vijana wenye umri mdogo ambao wanatumia Sheng, wanapokuja kwenye ofisi zetu kutafuta usaidizi. Ukiangalia pia kwenye sehemu zetu za uchuuzi, idadi kubwa ya wachuuzi ni watu ambao hawakuenda shule na hawafahamu Kiingereza. Wakienda sokoni kufanya biashara zao, wengi wao huenda na lugha ya asili kama vile Kikuyu, Kiluo, Kiluyhia na Kinandi. Wakiwa pale sokoni, inakuwa vigumu kufanya biashara kwa sababu hakuna lugha moja ambayo watu wanaweza kutumia kuwasiliana kuhusu mambo ya uchuuzi. Kulingana na mimi, Baraza la Kiswahili likibuniwa na Kiswahili kikiendelea kukuzwa, itakua ni njia moja ya kusaidia mawasiliano kwenye nafasi zetu za kazi. Mimi naunga mkono Hoja hii ya Mhe. Yusuf. Sheng ni lugha ambayo itakuja kunoga hapa Nairobi na huwa inabadilika kila mara. Wakati huu wanaongea hivi lakini baada ya miaka mitano, itakuwa imebadilika kwa kasi kikubwa sana. Kwa mfano, kitambo tulikuwa tunamuita Mhe. Yusuf kule mtaani bazenga lakini siku hizi vijana wanamuita mzimbitim . Hivyo ni vitu viwili ambavyo havieleweki. Lugha ya Sheng inafanya uhusiano kati ya wazazi na watoto wao kuwa mgumu. Hata kama watoto wanapanga mabaya, utakua katika maongezi yao lakini hutaelewa neno hata moja. Ukiangalia pia upande wa utamaduni, wakati tulipokuwa tukienda shuleni, tulikua na ubunifu wa hali ya juu katika sanii na uigizaji. Tulikuwa tunaona michezo mingi ya utamaduni kutoka kule Pwani. Kwa mfano, hivi majuzi kumekuwa na mchezo wa kuigiza uliokuwa ukiendele kwenye runinga, kuhusu Mekatilili wa Menza – ambao ulikuwa na mafunzo mengi sana ya utamaduni wa Mijikenda. Watu wengi walipitwa na utamaduni huu kwa sababu hawaelewi lugha ya Kiswahili. Itakuwa jambo la muhimu sana tukibuni Baraza la Kiswahili ili tuweze kurudisha ubunifu wa kitambo. Hii ni kama vile fasihi na michezo ya kuigiza zilivyokuwa, ili nchi yetu iweze kuendelea mbele vizuri. Kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki, nimekuwa mfanyibiashara Tanzania, Uganda, Congo, na kadhalika. Changamoto kubwa imekuwa ni mawasiliano. Mawasiliano kwenye biashara imekuwa ngumu sana kwa maana Kiswahili kinachotumika Uganda na Tanzania ni tofauti sana ni kile cha Congo. Ukiangalia historia, utapata kuwa asili ya Kiswahili ni Kenya. Lakini mataifa jirani yameweza kuchukulia Kiswahili kwa umaarufu mkubwa zaidi. Kwa mfano, hata Rais wa kule Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, wakati wa mazishi ya marehemu Mhe. Magufuli, alisema kuwa ataanzisha somo la Kiswahili katika shule za nchi yake. Lakini upande wetu, Kiswahili hakitiliwi maanani sana ilhali ni lugha ambayo imetupa umaarufu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki."
}