GET /api/v0.1/hansard/entries/1194844/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194844,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194844/?format=api",
    "text_counter": 159,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Tukiweza kubuni Baraza la Kiswahili, naamini tutaweza kupata maprofesa kama Ali Mazrui, ambaye alipata umaarufu wake kwa kukuza Kiswahili. Lugha ya Kiswahili inahifadhi sana mambo ya nidhamu. Inasemekana kuwa ukiongea lugha ya kigeni, unaongea kutoka kwa ubongo lakini ukiongea lugha ya asili unaongea kutoka kwa roho yako. Ndio maana kuna maneno ambayo unaweza kutumia rahisi sana kwa lugha ya Kiingereza lakini maneno hayo huwezi kusema mbele ya watu ukitumia lugha ya Kiswahili. Sitaki kutoa mfano lakini ni rahisi sana kusema kwa Kiingereza yale maneno ambayo tunasema ni wasio wa maadili lakini kwa Kiswahili inakuwa ni vigumu. Hii ni kwa sababu Kiswahili ina nidhamu zake. Ukiangalia pia kwa mitandao ya kijamii, kwa sasa hivi, lugha ya Kiswahili iko hali mahututi. Hii ni kwa sababu kwenye mitandao yote ya kijamii, kama vile WhatsApp, kama alivyosema Mhe. Didimus Barasa, kila mtu anatumia lugha ya Kimombo. Inaweza kuwa vyema Baraza la Kiswahili liweze kuangazia mambo kama hayo ili tuweze kurudisha umaarufu wa Kiswahili. Kwa hayo mengi, Mhe. Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Hoja hii ya kubuniwa kwa Baraza la Kiswahili katika taifa la Kenya. Naomba kumpa dadangu dakika zilizobaki."
}