GET /api/v0.1/hansard/entries/1194853/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194853,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194853/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika wa Muda, kama kuna jukumu moja muhimu ambalo Waziri aliyetwikwa jukumu hilo ako nalo saa hii, ni jukumu la kukuza Kiswahili humu nchini. Hivi sasa kuna jopo linalozunguka nchini kupokea maoni kutoka kwa washikadau kuhusu mfumo wa elimu wa CBC. Wakati utakapofika wa kuupiga msasa mtaala huu, tunafaa kuhakikisha kwamba lugha ya Kiswahili imechukua nafasi yake katika mpango wote wa elimu ya watoto wetu kuanzia PP1, ama gredi ya kwanza, ama elimu chekechea ndiyo mtoto akifika kiwango cha elimu ya juu awe ameifahamu vizuri lugha ya Kiswahili ndiyo hata akibahatika kuja Bungeni kama wanafunzi ambao wanatutembelea hapa, na kutazama mijadala, ajue kwamba Kiswahili ambacho watafunzwa pale mwanzo kwenye elimu chekechea, kwenye shule ya upili na hata kwenye chuo kikuu, ni kilekile Kiswahili ambacho kitatumika Bungeni."
}