GET /api/v0.1/hansard/entries/1194854/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194854,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194854/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, namuunga mkono Mhe. Yusuf na kumuhimiza kwamba asikomee hapa. Kwa sababu, kutokana na historia ya Bunge – mimi na wewe tumekuwa kwenye Mabunge ya 11 na 12, na sasa tuko katika Bunge la 13 – mengi ya maazimio tunayopitisha kupitia Miswada yanakwama wakati wa utekelezaji. Unabaki ukiyafuatilia kwenye Kamati ya Utekelezaji. Kwa hivyo, ninamhimiza Mhe. Yusuf kwamba ahakikishe kwamba pendekezo limeendelezwa hadi kuwa Mswada ili aulete Bungeni tuupitishe uwe sheria ndiyo suala hili liweze kupata uzito linalostahili na kutengewa bajeti kuhakikisha kwamba lengo letu limetimia. Hatuwezi kuwa tunasema tuko kwenye Umoja wa Afrika Mashariki bila ya kutekeleza maazimio ya umoja huo. Ukiaangalia Umoja wa nchi za Afrika, (AU) na UNESCO wameweza kukitambua Kiswahili. Lakini sisi wenyewe hatujaweza kubuni sheria ya kuliwesha jambo litendeke. Namhimiza Mhe. Yusuf kwamba, wakati hii Hoja itapitishwa katika na Bunge hili, asikwame hapo; angalie ni vipi tunawezakuendeleza mpaka iweze kuwa sheria ya nchi hii ndiyo tuwe kwenye msitari wa mbele kuhakikisha kwamba swala la kukikuza Kiswahili limewezekana. Mhe. Spka wa Muda, pia sisi, kama Wabunge, tujue kwamba tunapozungumza kuhusu usanifu wa lugha ( grammar) kama alivyosema Mheshimiwa mmoja, tunapaswa kuzingatia kanuni zote za lugha."
}