GET /api/v0.1/hansard/entries/1194858/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194858,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194858/?format=api",
    "text_counter": 173,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Gilgil, UDA",
    "speaker_title": "Mhe. Martha Wangari",
    "speaker": null,
    "content": " Ninaifuata, Mhe. Spika wa Muda. Ndiyo maana ninaweka baadhi ya maneno kwenye mabano; haswa maneno ambayo ninayatoa kwenye lugha ya Kimombo. Nataka kusema kwamba tujihimize sisi wenyewe kama Wabunge, tuitumie hii lugha, sio hapa tu kwenye Bunge, lakini hata kwa nyumba zetu na kwa jamii zetu ili tuweze kupata uzoefu wa ulimi. Hii ni kwa sababu hata miongoni mwetu sisi Bunge, kuna wanaosema kwamba huu Mswada haueleweki vizuri. Hawajazowea mambo ya Kiswahili. Tukiendelea kuzungumza Kiswahili, tutapata uzoefu wa kuzungumza na hatimaye hata wanaotutazama, wakiwemo watoto, wajue kwamba Kiswahili ni lugha yetu sisi sote, na inatumika nchini kwote, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na vile vile katika Afrika nzima. Kwa hayo mengi, ninaiunga mkono Hoja hii."
}