GET /api/v0.1/hansard/entries/1194864/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1194864,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194864/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ilani",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "BAKIZA. Tukiangalia katika kifungu cha saba cha Katiba ya Kenya, lugha mbili – Kizungu na Kiswahili – ndizo lugha rasmi humu nchini. Kwa hivyo, Mhe. Spika wa Muda, pendekezo hili la kubuniwa kwa Baraza la Kitaifa, kama alivyosema mwenzangu, Mhe. Martha, lisiwe Hoja pekee bali lifuatiliwe mpaka tubuni sheria kamili, na tuhakikishe kwamba Baraza hilo limetengewa bajeti yake. Vile vile, katika Bunge hili la 13, tusifanye mambo ya kawaida kama tulivyokuwa tukifanya katika Mabunge ya 12 na 11. Katika Mabunge yaliyopita, Hoja zinapitishwa lakini kutekelezwa inakuwa shida. Kwa hivyo, wakati huu ni muhimu Kamati ya Utekelezaji ( Committee on Implementation) ihakikishe kwamba masuala yote yatakayopitishwa hapa yanatekelezwa. Mhe. Spika awa Muda, jambo hili la Kiswahili ni jambo ambalo litaweza kuunganisha Afrika Mashariki nzima. Tukiangalia nchini Tanzania, wanaongea Kiswahili. Waganda pia wanaongea Kiswahili. Na njia hii ya Kiswahili ndio itafanya iwe rahisi kwa watu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya biashara na kuleta undugu. Tunajua kwamba hivi karibuni ndugu zetu wa kule Congo pia wamejiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukiangalia Congo pia, watu wanazungumza Kiswahili. Ijapokuwa Kiswahili cha kule, kidogo ni tofauti na Kiswahili chetu. Kwa mfano, utamsikia Mkongo akisema, “Mimi nikiwa Papa Fulungenge, nasema kuwa batoto ba Congo na batoto ba Kenya, bote ni batoto bamoja. ” Hivyo ndivyo Wakongo wanavyozungumza. Sote basi ni watu wamoja, Wakenya na vile vile Wakongo. Mhe. Spika wa Muda, kubuniwa kwa baraza hili la kitaifa kutaweza kufanya biashara na mawasiliano kuwa rahisi katika nchi hizi zetu. Tunaona katika Vifungu cha 119 na 137, vya Mkataba wa Uanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vimewajibisha mataifa wanachama kustawisha na kuendeleza Kiswahili kama lugha ya mshikamano wa nchi wanachama. Kwa hivyo, Mheshimiwa, ukiangalia jambo kama hili limeweza kueneza ubora wa kuinua Kiswahili. Miongoni mwa jamii za Afrika Mashariki kuna lahaja mbali mbali za Kiswahili, ikiwemo Kijomvu, lakini hakuna Wajomvu. Mhe. Spika wa Muda, naona wafurahi, wacheka lakini wako Wajomvu. Mimi najifuharisha na nafurahi kuwa ni mmoja wa hao Wajomvu. Leo hii, utamuona Mswahili wa Kijomvu akitaka kutoa mfano wa watoto wawili ambao wanacheza na kwa bahati mbaya mmoja anamchoma kisu kwa jicho mwingine. Mjomvu husema, “Huyu mwana mkunzu unamtopoa,” yaani maana yake ni kuwa huyu ameweza kumkwaza mwingine kwenye jicho. Na vile vile, wakiogelea baharini, utawaskia wakisema, “Mwana huyu anaoga kutoka uta tauta katika pwani hii.” Kwa haya yote twajivunia kwa sababu hii ni lugha yetu. Na leo Kijomvu nakizungumza katika Bunge la Kenya. Kwa hivyo, ninafurahi kuwa Kijomvu ni moja ya lahaja za Kiswahili. Na punde, kama alivyosema… Ndipo ukaona Mhe. Martha akizungumza Kiswahili kidogo. Nilijua ni yeye kwa sababu uswahili ulikuwa umemnogea mpaka nikaona nikama ambaye anatoka Pwani. Ukienda Dar-es-Salaam, utapata kwamba katika maeneo mengi sana, hata kama kunawekwa mabango yoyote pale, utapata yanaandikwa kwa lugha ya Kiswahili. Wanajivunia lugha yao ya Kiswahili. Mawasiliano mazuri yatainua biashara na ajira Afrika Mashariki. Hii ni kwa sababu ni Baraza zima ambalo linahitaji huduma kwa watu kulishughulikia. Nampongeza sana Mhe. Yussuf Hassan kwa kuleta Hoja hii katika Bunge hili."
}