GET /api/v0.1/hansard/entries/1194865/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1194865,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1194865/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ilani",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nitakuambia mambo ya maajabu. Kati ya makabila madogo madogo 12 kule Mombasa, kuna makabila madogo ambayo kwa kimombo tunayaita minority tribes . Hayajulikani. Nataka kutaja katika kumbukumbu kwa kumpongeza kamishna mmoja wa polisi anayeitwa Murshid. Wakati uajiri wa polisi ulipofanyika katika sehemu yangu mwaka wa 2014, kuna mtoto mmoja wa Jomvu alitolewa kwa hesabu kwa sababu kabila yake haikuwa inajulikana. Nilipiga kelele kama Mbunge na nikafikisha barua kwa kamishna wa wakati ule. Ilidhibitika kuwa hiyo ndiyo moja katika kabila yenyeji ambayo inaishi sehemu hizo. Huyo mtoto alichukuliwa kama polisi. Leo hii anahudumia kitengo cha Kenya Police. Ni mtoto wa Mzee Salim."
}